TINGA TINGA KUFANYA MAONYESHO JAPAN

PICHA 35 za wasanii wa sanaa ya uchoraji katika kampuni ya Tingatinga zinatarajiwa kufanyiwa maonesho nchini Japan Oktoba 21 hadi Novemba 20 mwaka huu.
Maonesho hayo yatafanyika katika mji wa Fukuhoka Oktoba 21 hadi 30 wakati katika mji wa Sapporo yatafanyika Novemba 11 hadi 20.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kampuni ya Baraka iliyoko nchini Japan, Tsuyoshi Shimaoka alisema lengo la maonesho hayo ni kueneza mila na desturi za Watanzania nchini humo.
Alisema mbali na maonesho hayo pia  watakwenda katika shule za Shibetsu Junior High School, Sapporo Chuo Primary, Juniour High School pamoja na Hikizu Primary School ili kutoa elimu hiyo kwa wanafunzi (Curture Exchange).
Shimaoka alisema Japan wanaamini kuwa Afrika ni Bara la njaa, magonjwa na ni sehemu ambayo wanaishi watu weusi pekee, hivyo elimu hiyo itakayotolewa kupitia picha itasaidia kuondoa fikra hizo potofu.
Alisema katika maonyesho hayo kutakuwa na sanaa ya uchoraji (live painting) itakayofanywa na Makamu Mwenyekiti wa Tinga tinga, Abbasy Mbuka.
Pia alisema kuwa asilimia 10 yatapato yatakayopatikana katika mauzo ya picha hizo itapelekwa katika kituo kinachoshughulikia watu wa maafa ya Tsunami kutokana na mpaka sasa wengi wao hawana makazi na chakula.
Alisema hatua hiyo pia imeafikiwa na Balozi wa Tanzania nchini Japan, Salome Sijaona pamoja na watu wa Japani ambapo tayari vyombo vya Habari nchini humo vimetangaza kuwepo kwa maonyesho hayo.
Wasanii hao ambao picha zao zimechukuliwa ni pamoja na Omar Amonde aliyefundishwa sanaa ya uchoraji na marehemu Tingatinga, Beka Wasiya, Mustafa Yusuph, Abdallah Said, Shaaban Ramadhani, Rajab Duke, Said Omar, Rukas Ndunguru, Rabuni Rashid, Mohammed Charinda, Zabur Chimwanda, Aminata Rashid, Darin Charinda, Mwatuka Salum, Abdul Mkura, Noel Kambiri, Baroni Mrope, Said Nakope, Abdullahman Hassan.
Wengine ni Abbasy Nandiwi, Daudi Tingatinga, Said Mteko, Jafari Mims, Ngayo Peter, Shaaban Mkalekwa, Mourus Marikita, Godfrey Thiamar, Hemed Mbaruk, Omar Sdogo, Mohammed Chiwaya na marehemu Sayuki Sayuki ambaye picha zake bado zipo.

Comments

Popular Posts